6. Waamuzi mahakamani atawaongoza kutenda haki,nao walinzi wa mji atawapa nguvu.
7. Lakini wako wengine waliolewa divaina kuyumbayumba kwa sababu ya pombe;naam, makuhani na manabii wamelewa mvinyo,wamevurugika kwa divai.Wanayumbayumba kwa pombe kali;maono yao yamepotoka,wanapepesuka katika kutoa hukumu.
8. Meza zote zimetapakaa matapishi,hakuna mahali popote palipo safi.
9. Wao wananidhihaki na kuuliza:“Huyu nabii ataka kumfundisha nani?Je, anadhani atatueleza sisi ujumbe wake?Je, sisi ni watoto wachangawalioachishwa kunyonya juzijuzi?
10. Anatufundisha kama watoto wadogo:Sheria baada ya sheria,mstari baada ya mstari;mara hiki, mara kile!”
11. Haya basi!Mwenyezi-Mungu ataongea na watu hawakwa njia ya watu wa lugha tofautiwanaoongea lugha ngeni.
12. Hata hivyo yeye alikuwa amewaahidi:“Nitawaonesheni pumziko,nitawapeni pumziko enyi mliochoka.Hapa ni mahali pa pumziko.”Lakini wao hawakutaka kunisikiliza.