26. Mtu huyo huwa anajua la kufanya,kwa sababu Mungu wake humfundisha.
27. Bizari haipurwi kwa mtarimbowala jira kwa gari la ng'ombe!Ila bizari hupurwa kwa kijitina jira kwa fimbo.
28. Mkulima apurapo ngano yake,haendelei kuipura mpaka kuvunja punje zake.Anajua jinsi ya kuipura kwa gurudumu,bila kuziharibu punje za ngano.