Isaya 28:13-18 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Kwa hiyo kwao neno la Mwenyezi-Mungu litakuwa tu:Sheria sheria, mstari mstari;mara hiki, mara kile!Nao watalazimika kukimbialakini wataanguka nyuma;watavunjika, watanaswa na kutekwa.

14. Basi, sikilizeni neno la Mwenyezi-Mungu,enyi wenye madharau mnaotawala watu wa Yerusalemu,

15. “Nyinyi mnajidai mmefanya mkataba na kifo,mmefanya mapatano na Kuzimu!Nyinyi mwasema eti balaa lijapo halitawapata,kwa sababu mmefanya uongo kuwa tegemeo lenu,na udanganyifu kuwa kinga yenu!”

16. Basi, hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi-Mungu:“Tazama! Naweka mjini Siyoni jiwe la msingi,jiwe ambalo limethibitika.Jiwe la pembeni, la thamani,jiwe ambalo ni la msingi thabiti;jiwe lililo na maandishi haya:‘Anayeamini hatatishika.’

17. Nitatumia haki kama kipimo changu,nitatumia uadilifu kupimia.”Mvua ya mawe itaufagilia mbali uongo mnaoutegemea,na mafuriko yataharibu kinga yenu.

18. Hapo mkataba wenu na kifo utabatilishwa,na mapatano yenu na Kuzimu yatafutwa.Janga lile kuu litakapokujalitawaangusheni chini.

Isaya 28