Isaya 26:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Siku ile watu wataimba wimbo huu katika nchi ya Yuda:Sisi tuna mji imara:Mungu anatulinda kwa kuta na ngome.

2. Fungueni malango ya mji,taifa aminifu liingie;taifa litendalo mambo ya haki.

3. Ee Mungu, wawaweka katika amani walio thabiti,wawaweka katika amani kwa kuwa wanakutegemea.

4. Mtumaini Mwenyezi-Mungu siku zotekwa maana yeye ni mwamba wa usalama milele.

5. Amewaporomosha waliokaa pande za juu,mji maarufu ameuangusha mpaka chini,ameutupa mpaka mavumbini.

6. Sasa mji huo unakanyagwakanyagwakwa miguu ya watu maskini na fukara.

7. Njia ya watu wanyofu ni rahisi;ewe Mungu mwadilifu, wasawazisha njia yao.

Isaya 26