Isaya 24:20-23 Biblia Habari Njema (BHN)

20. Inapepesuka kama mlevi,inayumbayumba kama kibanda.Imelemewa na mzigo wa dhambi zakenayo itaanguka wala haitainuka tena.

21. Siku ile Mwenyezi-Mungu ataliadhibu jeshi la anganikadhalika na wafalme wa duniani.

22. Wote watakusanywa kama wafungwa shimoni;watafungwa gerezani pamoja kwa miaka mingi,na baada ya muda huo atawaadhibu.

23. Kisha mwezi utaaibishwa,nalo jua litaona aibu kuangaza,kwa kuwa Mwenyezi-Mungu wa majeshiatatawala huko Yerusalemu katika mlima Siyoni;ataonesha wazee wa watu wake utukufu wake.

Isaya 24