1. Kauli ya Mungu dhidi ya Tiro.Ombolezeni, enyi mabaharia wa mbali baharini,maana Tiro mji wenu umeharibiwa,humo hamna tena makao wala bandari.Mtazipokea habari hizo mtakaporejea kutoka Kupro.
2. Nyamazeni kwa mshangao enyi wakazi wa pwani,naam, tulieni enyi wafanyabiashara wa Sidoni,ambao wajumbe wenu wanapita baharini,
3. wakasafiri katika bahari nyingi.Mapato yenu yalikuwa nafaka ya Misri,mkaweza kufanya biashara na mataifa.