Isaya 21:3-10 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Kwa maono hayo nimeingiwa na hofu kubwa,uchungu mwingi umenikumba;kama uchungu wa mama anayejifungua.Maumivu yamenizidi hata siwezi kusikia;nimefadhaika hata siwezi kuona.

4. Moyo unanidunda na woga umenikumba.Nilitamani jioni ifikelakini ilipofika ikawa ya kutetemesha.

5. Chakula kimetayarishwa,shuka zimetandikwa,sasa watu wanakula na kunywa.Ghafla, sauti inasikika:“Inukeni enyi watawala!Wekeni silaha tayari!”

6. Maana Bwana aliniambia,“Nenda ukaweke mlinzi;mwambie atangaze atakachoona.

7. Akiona kikosi, wapandafarasi wawiliwawili,wapandangamia na wapandapunda,na awe macho;naam, akae macho!”

8. Kisha huyo mlinzi akapaza sauti:“Bwana, nimesimama juu ya mnara wa ulinzi mchana kutwa,nimeshika zamu usiku kucha!”

9. Tazama, kikosi kinakuja,wapandafarasi wawiliwawili.Wanasema: “Babuloni umeanguka! Umeanguka!Sanamu zote za miungu yakezimetupwa chini na kuvunjwavunjwa!”

10. Ewe Israeli, watu wangu,enyi mliotwangwa na kupurwa kama nafaka.Sasa nimewaambieni mambo niliyoyasikiakwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli.

Isaya 21