Isaya 17:4-7 Biblia Habari Njema (BHN)

4. “Siku hiyo, fahari ya Yakobo itaporomoshwa,na unono wake ataupoteza.

5. Atakwisha kama shamba lililovunwa,atafanyiwa kama mvunaji avunavyo nafaka,atakuwa kama shamba lililovunwa bondeni Refaimu.

6. Atabakiziwa wachache kama vile baada ya zeituni:Zeituni mbili, tatu katika tawi la juu;nne, tano katika matawi ya mti uzaao sana.Mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nimenena.”

7. Siku hiyo, watu watamwangalia Muumba wao, na kuelekeza macho yao kwa huyo Mtakatifu wa Israeli.

Isaya 17