Isaya 14:22-28 Biblia Habari Njema (BHN)

22. Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Nitaushambulia mji wa Babuloni na kuuangamiza kabisa. Nitaharibu kila kitu, mji wote, watoto na yeyote aliyebaki hai. Mimi Mwenyezi-Mungu nimenena.

23. Nitaufanya kuwa makao ya nungunungu, na utakuwa madimbwi ya maji. Nami nitaufagilia mbali kwa ufagio wa maangamizi. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimenena.”

24. Mwenyezi-Mungu wa majeshi ameapa:“Kama nilivyopanga,ndivyo itakavyokuwa;kama nilivyokusudia,ndivyo itakavyokamilika.

25. Nitauvunja uwezo wa Waashuru nchini mwangu;nitawakanyagakanyaga katika milima yangu.Nitawaondolea watu wangu nira ya dhuluma yao,na mzigo wa mateso yao.”

26. Huu ndio uamuzi wake Mwenyezi-Mungukuhusu dunia yote;hii ndiyo adhabu atakayotoajuu ya mataifa yote.

27. Kama Mwenyezi-Mungu wa majeshi ameamua,nani atakayeweza kubatilisha uamuzi wake?Kama amepania kutoa adhabu,ni nani atakayempinga?

28. Mwaka alipofariki mfalme Ahazi, Mungu alitoa kauli hii:

Isaya 14