21. Kaeni tayari kuwachinja watoto wakekwa sababu ya makosa ya baba zao,wasije wakaamka na kuimiliki nchi,na kuijaza dunia yote miji yao.”
22. Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Nitaushambulia mji wa Babuloni na kuuangamiza kabisa. Nitaharibu kila kitu, mji wote, watoto na yeyote aliyebaki hai. Mimi Mwenyezi-Mungu nimenena.
23. Nitaufanya kuwa makao ya nungunungu, na utakuwa madimbwi ya maji. Nami nitaufagilia mbali kwa ufagio wa maangamizi. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimenena.”
24. Mwenyezi-Mungu wa majeshi ameapa:“Kama nilivyopanga,ndivyo itakavyokuwa;kama nilivyokusudia,ndivyo itakavyokamilika.
25. Nitauvunja uwezo wa Waashuru nchini mwangu;nitawakanyagakanyaga katika milima yangu.Nitawaondolea watu wangu nira ya dhuluma yao,na mzigo wa mateso yao.”
26. Huu ndio uamuzi wake Mwenyezi-Mungukuhusu dunia yote;hii ndiyo adhabu atakayotoajuu ya mataifa yote.
27. Kama Mwenyezi-Mungu wa majeshi ameamua,nani atakayeweza kubatilisha uamuzi wake?Kama amepania kutoa adhabu,ni nani atakayempinga?
28. Mwaka alipofariki mfalme Ahazi, Mungu alitoa kauli hii: