Isaya 13:10-18 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Nyota na vilimia vyake angani hazitaangaza;jua linapochomoza litakuwa giza,na mwezi hautatoa mwanga wake.

11. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Nitauadhibu ulimwengu kwa uovu wake,waovu kwa sababu ya makosa yao.Nitakikomesha kiburi cha wenye majivuno,na kuporomosha ubaradhuli wa watu katili.

12. Nitawafanya watu kuwa wachache kuliko dhahabu safi;binadamu watakuwa wachache kuliko dhahabu ya Ofiri.

13. Nitazitetemesha mbingunayo nchi itatikisika katika misingi yakekwa sababu ya ghadhabu yangu Mwenyezi-Mungusiku ile ya hasira yangu kali.

14. “Kama swala anayewindwa,kama kondoo wasio na mchungaji,kila mmoja atajiunga na watu wakekila mtu atakimbilia nchini mwake.

15. Yeyote atakayeonekana atatumbuliwa,atakayekamatwa atauawa kwa upanga.

16. Watoto wao wachanga watapondwapondwa mbele yao,watanyanganywa nyumba zao,na wake zao watanajisiwa.

17. “Ninawachochea Wamedi dhidi yao;watu ambao hawajali fedhawala hawavutiwi na dhahabu.

18. Mishale yao itawaua vijana,hawatakuwa na huruma kwa watoto,wala kuwahurumia watoto wachanga.

Isaya 13