1. Basi, waiteni kaka zenu, “Watu wangu,” na dada zenu, “Waliohurumiwa.”
2. Mlaumuni mama yenu mlaumuni,maana sasa yeye si mke wanguwala mimi si mume wake.Mlaumuni aondokane na uasherati wake,ajiepushe na uzinzi wake.
3. La sivyo, nitamvua nguo abaki uchi,nitamfanya awe kama alivyozaliwa.Nitamfanya awe kama jangwa,nitamweka akauke kama nchi kavu.Nitamuua kwa kiu.
4. Na watoto wake sitawahurumia,maana ni watoto wa uzinzi.
5. Mama yao amefanya uzinzi,aliyewachukua mimba amefanya mambo ya aibu.Alisema; “Nitaambatana na wapenzi wangu,ambao hunipa chakula na maji,sufu na kitani, mafuta na divai.”
6. Basi, nitaiziba njia yake kwa miiba,nitamzungushia ukuta,asipate njia ya kutokea nje.