3. Ashuru haitatuokoa,hatutategemea tena farasi wa vita.Hatutaviita tena: ‘Mungu wetu’hivyo vinyago tulivyochonga wenyewe.Kwako ee Mungu yatima hupata huruma.”
4. Mwenyezi-Mungu asema,“Nitaponya utovu wao wa uaminifu;nitawapenda tena kwa hiari yangu,maana sitawakasirikia tena.
5. Nitakuwa kama umande kwa Waisraelinao watachanua kama yungiyungi,watakuwa na mizizi kama mwerezi wa Lebanoni.
6. Chipukizi zao zitatanda na kuenea,uzuri wao utakuwa kama mizeituni,harufu yao nzuri kama maua ya Lebanoni.