Hosea 13:4-10 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Mwenyezi-Mungu asema:“Lakini mimi, Mwenyezi-Mungu, ni Mungu wenu,ambaye niliwatoa nchini Misri;hamna mungu mwingine ila mimi,wala hakuna awezaye kuwaokoeni.

5. Ni mimi niliyewatunza mlipokuwa jangwani,katika nchi iliyokuwa ya ukame.

6. Lakini mlipokwisha kula na kushiba,mlianza kuwa na kiburi, mpaka mkanisahau.

7. Basi, nitakuwa kama simba kwenu nyote;nitawavizieni kama chui njiani.

8. Nitawarukieni kama dubualiyenyang'anywa watoto wake.Nitawararua vifua vyenuna kuwala papo hapo kama simba;nitawararua vipandevipande kama mnyama wa porini.

9. “Nitawaangamiza, enyi Waisraeli.Nani ataweza kuwasaidia?

10. Yuko wapi sasa mfalme wenu awaokoe?Wako wapi wale wakuu wenu wawalinde?Nyinyi ndio mlioomba:‘Tupatie mfalme na wakuu watutawale.’

Hosea 13