1. Watu wa Efraimu wananirundikia uongo,na Waisraeli udanganyifu.Watu wa Yuda, wananiasi mimi Mungu Mtakatifu.
2. “Watu wa Efraimu wanachunga upepokutwa nzima wanafukuza upepo wa mashariki.Wanazidisha uongo na ukatili,wanafanya mkataba na Ashuruna kupeleka mafuta Misri.”
3. Mwenyezi-Mungu ana mashtaka dhidi ya Yuda;atawaadhibu wazawa wa Yakobo kadiri ya makosa yao,na kuwalipa kadiri ya matendo yao.