Hesabu 4:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwenyezi-Mungu akawaambia Mose na Aroni,

2. “Wahesabu watu wa ukoo wa Kohathi, mmoja wa koo za Lawi, kufuatana na jamaa zao na koo zao;

3. utawaorodhesha wanaume wote wenye umri kati ya miaka thelathini na hamsini wanaofaa kujiunga na huduma ya hema la mkutano.

Hesabu 4