12. halafu utateremka kufuata mto Yordani hadi Bahari ya Chumvi; hii ndiyo itakuwa nchi yako kama mpaka ulivyo.”
13. Basi, Mose akawaambia Waisraeli, “Hii ndiyo nchi mtakayoirithi kwa kupiga kura, nchi ambayo Mwenyezi-Mungu ameagiza yapewe makabila tisa na nusu.
14. Kabila la Reubeni na la Gadi, na nusu ya kabila la Manase yamepata urithi wao kulingana na koo zao.
15. Makabila hayo mawili na nusu yamepata urithi wao ngambo ya mto Yordani upande wa mashariki, mkabala wa Yeriko, mawioni.”
16. Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose,
17. “Kuhani Eleazari na Yoshua mwana wa Nuni ndio watakaowagawia watu nchi kuwa mali yao.
18. Utachukua pia kiongozi mmoja kutoka kila kabila kusaidia katika ugawaji wa nchi.
19. Haya ndiyo majina yao:Kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune.
20. Kabila la Simeoni, Shemueli mwana wa Amihudi.
21. Kabila la Benyamini, Elidadi mwana wa Kisloni.
22. Kabila la Dani, Buki mwana wa Yogli.
23. Kabila la Manase mwanawe Yosefu, Hanieli mwana wa Efodi.
24. Kabila la Efraimu, mwanawe Yosefu, Kemueli mwana wa Shiftani.
25. Kabila la Zebuluni, Elisafani mwana wa Parnaki.
26. Kabila la Isakari, Paltieli mwana wa Azani.
27. Kabila la Asheri, Ahihudi mwana wa Shelomi
28. Kabila la Naftali, Pedaheli mwana wa Amihudi.