Hesabu 34:1-12 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose,

2. “Waamuru Waisraeli ukisema: Mtakapoingia Kanaani, nchi ambayo ninawapa iwe nchi yenu, mipaka ya eneo lenu lote itakuwa kama ifuatavyo.

3. Upande wa kusini mpaka wenu utakuwa kutoka jangwa la Sini kupitia upande wa Edomu. Utaanzia mashariki upande wa kusini mwisho wa Bahari ya Chumvi.

4. Kisha utapinda kusini kuelekea pito la Akrabimu na kupitia Sini hadi Kadesh-barnea, upande wa kusini. Kutoka hapo, mpaka utapinda kuelekea kaskazini-magharibi hadi Hasar-adari na kupita hadi Azmoni.

5. Kutoka Azmoni utapinda kuelekea kijito cha Misri kwenye mpaka wa Misri na kuishia bahari ya Mediteranea.

6. “Mpaka wenu wa upande wa magharibi utakuwa bahari ya Mediteranea.

7. “Mpaka wenu wa upande wa kaskazini utakuwa kama ifuatavyo: Kutoka bahari ya Mediteranea, mtatia alama hadi Mlima Hori.

8. Kutoka Mlima Hori mtatia alama hadi pito la Hamathi, na kuendelea hadi Sedadi,

9. na kupita hadi Zifroni na kuishia Hazar-enani; huo utakuwa mpaka wenu wa kaskazini.

10. “Mpaka wenu wa upande wa mashariki mtauweka kutoka Hazar-enani hadi Shefamu.

11. Kutoka Shefamu utaelekea kusini hadi Ribla, mashariki mwa Aini; kisha mpaka huo utakwenda chini hadi mteremko wa mashariki wa ziwa Kinerethi,

12. halafu utateremka kufuata mto Yordani hadi Bahari ya Chumvi; hii ndiyo itakuwa nchi yako kama mpaka ulivyo.”

Hesabu 34