Hesabu 33:42-51 Biblia Habari Njema (BHN)

42. Kutoka Salmona, walipiga kambi yao Punoni.

43. Kutoka Punoni, walipiga kambi yao Obothi.

44. Kutoka Obothi, walipiga kambi yao Iye-abarimu, katika eneo la Moabu.

45. Kutoka Iye-abarimu, walipiga kambi yao Dibon-gadi.

46. Kutoka Dibon-gadi, walisafiri na kupiga kambi yao Almon-diblathaimu.

47. Kutoka Almon-diblathaimu, walisafiri na kupiga kambi yao katika milima ya Abarimu, karibu na Mlima Nebo.

48. Kutoka milima ya Abarimu, walisafiri na kupiga kambi yao katika tambarare za Moabu ngambo ya mto Yordani karibu na Yeriko.

49. Walipiga kambi hiyo karibu na mto Yordani kati ya Beth-yeshimothi na bonde la Abel-shitimu kwenye tambarare za Moabu.

50. Katika tambarare za Moabu, ngambo ya mto Yordani karibu na Yeriko, Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose,

51. “Waambie Waisraeli kwamba mtakapovuka mto Yordani na kuingia katika nchi ya Kanaani,

Hesabu 33