47. Hizo ndizo koo za kabila la Asheri, jumla wanaume 53,400.
48. Kabila la Naftali lilikuwa na jamaa za Yaseeli, Guni,
49. Yeseri na Shilemu.
50. Hizi ndizo koo za kabila la Naftali, jumla wanaume 45,400.
51. Idadi ya wanaume Waisraeli waliohesabiwa ilikuwa 601,730.
52. Kisha Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose,
53. “Makabila haya yatagawiwa nchi iwe urithi wao, kulingana na idadi ya majina yao.