18. Edomu itamilikiwa naye,Seiri itakuwa mali yake,Israeli itapata ushindi mkubwa.
19. Mmoja wa wazawa wa Yakobo atatawalanaye atawaangamiza watakaonusurika wa Ari.”
20. Kisha Balaamu akawaangalia Waamaleki, akatoa kauli hii:“Amaleki ni taifa lenye nguvu kuliko yote,lakini mwishoni litaangamia kabisa.”