Hesabu 22:6-10 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Njoo sasa uwalaani watu hawa kwa ajili yangu maana wana nguvu kuliko mimi. Labda nitaweza kuwashinda na kuwafukuza wasiingie katika nchi yangu, kwa maana najua kuwa wewe ukimbariki mtu hubarikiwa, ukimlaani mtu hulaaniwa.”

7. Basi, maofisa wa Moabu na Midiani wakachukua ada ya mwaguzi, wakaondoka kwenda kwa Balaamu. Walipowasili, walimpa Balaamu ujumbe wa Balaki.

8. Balaamu akawaambia, “Laleni huku usiku huu, nami nitawajulisheni atakayoniambia Mwenyezi-Mungu.” Basi, wazee hao wa Moabu wakakaa na Balaamu.

9. Kisha Mungu alimjia Balaamu, akamwuliza, “Ni nani hawa wanaokaa nawe?”

10. Balaamu akamjibu Mungu, “Balaki mwana wa Sipori amenipelekea ujumbe kwamba

Hesabu 22