Hesabu 12:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kisha Miriamu na Aroni walianza kumsema vibaya Mose kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa.

2. Wakasema, “Hivi kwani Mwenyezi-Mungu amezungumza kwa kumwagiza Mose peke yake? Je, hajazungumza nasi pia?” Mwenyezi-Mungu aliyasikia maneno hayo.

3. (Mose alikuwa mtu mnyenyekevu kuliko watu wengine wote waliokuwa duniani.)

4. Halafu ghafla, Mwenyezi-Mungu akawaambia Mose, Aroni na Miriamu, “Njoni katika hema la mkutano, nyinyi watatu.” Basi, wote watatu wakaenda kwenye hema la mkutano.

5. Hapo Mwenyezi-Mungu akashuka katika nguzo ya wingu, akasimama kwenye mlango wa hema, akawaita Aroni na Miriamu. Wote wawili wakasogea mbele.

Hesabu 12