1. Mnamo siku ya kwanza ya mwezi wa pili, mwaka wa pili baada ya wana wa Israeli kutoka Misri, Mwenyezi-Mungu aliongea na Mose ndani ya hema la mkutano jangwani Sinai, akamwambia hivi:
2. “Wewe na Aroni fanyeni sensa ya jumuiya yote ya Waisraeli, familia mojamoja kwa kufuata koo zao na idadi ya majina yao kila mwanamume mmojammoja;
3. wale wote katika Israeli wanaoweza kwenda vitani, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, mtawaweka katika orodha ya vikosi vikosi.