19. Ole wake mtu aliambiaye gogo: ‘Amka!’Au jiwe bubu ‘Inuka!’Je, sanamu yaweza kumfundisha mtu?Tazama imepakwa dhahabu na fedha,lakini haina uhai wowote.”
20. Lakini Mwenyezi-Mungu yumo katika hekalu lake takatifu;dunia yote na ikae kimya mbele yake.