7. Wao ni watu wa kuchukiza na kutisha;wao hujiamulia wenyewe nini haki na adhama.
8. “Farasi wao ni wepesi kuliko chui;wakali kuliko mbwamwitu wenye njaa.Wapandafarasi wao wanatoka mbali,wanaruka kasi kama tai arukiavyo mawindo.
9. “Wote wanakuja kufanya ukatili;kwa nyuso kakamavu wanasonga mbele,wanakusanya mateka wengi kama mchanga.
10. Wanawadhihaki wafalme,na kuwadharau watawala.Kila ngome kwao ni mzaha,wanairundikia udongo na kuiteka.
11. Kisha wanasonga mbele kama upepo,wafanya makosa na kuwa na hatia,maana, nguvu zao ndizo mungu wao!”