Ezekieli 5:15-17 Biblia Habari Njema (BHN)

15. Utakuwa kitu cha dharau na aibu, mfano wa kitu cha kuchukiza kwa makabila yanayokuzunguka, wakati nitakapotekeleza hukumu zangu dhidi yako kwa hasira na ghadhabu yangu kali. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

16. Wakati huo nitaiachilia mishale yangu mikali ya njaa iwachome na kuangamiza wakazi wako. Nitawafanya wafe njaa kwa kuiharibu akiba yao ya chakula.

17. Nitakupelekea njaa na wanyama wakali ambao watakupokonya watoto wako; maradhi mabaya, mauaji, na vita vitakuja kukuangamiza. Mimi, Mwenyezi-Mungu, nimesema.”

Ezekieli 5