Ezekieli 42:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kisha yule mtu alinipeleka kwenye uwanja wa nje hadi kwenye jengo lililokuwa upande wa kaskazini, naye akaniingiza kwenye vyumba vilivyokabili ua wa hekalu na jengo lililokuwa upande wa kaskazini.

2. Jengo hili lililokuwa upande wa kaskazini lilikuwa na urefu wa mita 50 na upana wa mita 25.

Ezekieli 42