Ezekieli 37:23-28 Biblia Habari Njema (BHN)

23. Hawatajitia unajisi tena kwa sanamu za miungu yao na kwa mambo yao ya kuchukiza wala kwa makosa yao. Nitawaokoa wasiwe tena waasi. Nao watakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wao.

24. Mtumishi wangu Daudi atakuwa mfalme wao; naam, watakuwa na mchungaji mmoja tu. Watayafuata maagizo yangu na kuzingatia kanuni zangu.

25. Watakaa katika nchi ya wazee wao ambayo nilimpa Yakobo. Wao na watoto wao na wajukuu wao wataishi humo milele. Naye Daudi, mtumishi wangu, atakuwa mtawala milele.

26. Nitafanya nao agano la amani, nalo litakuwa agano la milele. Nitawabariki na kuwafanya wawe wengi, na maskani yangu nitaiweka kati yao milele.

27. Nitaishi kati yao; nitakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wangu.

28. Nayo mataifa yatatambua kuwa mimi Mwenyezi-Mungu, nimewatakasa Waisraeli na kwamba maskani yangu ipo kati yao milele.”

Ezekieli 37