25. Mwenyezi-Mungu akaniambia, “Wewe mtu! Siku ile nitakapoondoa kwao hicho ambacho ni tegemeo lao, na sababu ya shangwe yao, mahali ambapo wanapenda sana kupaona, nitawaondoa watoto wao wa kiume na wa kike.
26. Siku hiyo, mtu atakayeokoka atakuja kukupasha habari hizo.
27. Siku hiyohiyo, utaacha kuwa bubu, nawe utaweza kuongea naye. Kwa hiyo wewe utakuwa ishara kwao, nao watatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”