Ezekieli 16:61-63 Biblia Habari Njema (BHN)

61. Nawe utakumbuka mienendo yako na kuona aibu wakati nitakapokupa dada zako, mkubwa na mdogo, kama binti zako, ingawa si kwa sababu ya agano kati yangu na wewe.

62. Mimi nitafanya agano nawe, nawe utatambua kwamba mimi ni Mwenyezi-Mungu.

63. Nitakusamehe kila kitu ulichotenda. Nawe utakapokumbuka hayo yote uliyotenda utashangaa na kunyamaza kwa aibu wala hutathubutu kusema tena. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Ezekieli 16