Amosi 9:4-8 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Wajapochukuliwa mateka na adui zao,huko nitatoa amri wauawe kwa upanga.Nitawachunga kwa makini sananiwatendee mabaya na si mema.”

5. Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi,anaigusa ardhi nayo inatetemekana wakazi wake wanaomboleza;dunia nzima inapanda na kushukakama kujaa na kupwa kwa mto Nili wa Misri.

6. Mwenyezi-Mungu amejenga makao yake mbinguni,nayo dunia akaifunika kwa anga;huyaita maji ya bahari,na kuyamwaga juu ya nchi kavu.Mwenyezi-Mungu, ndilo jina lake!

7. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Kwangu mimi, nyinyi Waisraeli,hamna tofauti yoyote na watu wa Kushi!Niliwatoa Wafilisti kutoka Krete,na Waashuru kutoka Kiri,kama nilivyowatoa nyinyi kutoka Misri.

8. Mimi, Bwana Mwenyezi-Mungu nautazama ufalme wenye dhambi,na nitauangamiza kabisa kutoka duniani.Lakini sitawaangamiza wazawa wote wa Yakobo.

Amosi 9