9. Huko vilimani ambako wazawa wa Isaka hutambikia,kutafanywa kuwa uharibifu mtupuna maskani ya Waisraeli yatakuwa magofu.Nitaushambulia kwa vita ukoo wa mfalme Yeroboamu.”
10. Basi, Amazia kuhani wa mji wa Betheli, akampelekea mfalme Yeroboamu wa Israeli habari hizi: “Amosi analeta fitina juu yako katika ufalme wa Israeli. Hotuba zake ni hatari kwa nchi hii.
11. Anachosema ni hiki:‘Yeroboamu atakufa kwa upanganao Waisraeli watapelekwa uhamishoni,mbali kabisa na nchi yao.’”
12. Kisha Amazia akamwambia Amosi, “Sasa tumekuchoka, ewe nabii! Nenda zako! Rudi katika nchi ya Yuda, ukatoe unabii huko upate na ujira wako hukohuko.
13. Usitoe tena unabii hapa mjini Betheli, kwa kuwa hapa ni maskani ya ibada ya mfalme; ni hekalu la utawala huu.”
14. Amosi akamjibu Amazia, “Mimi si nabii wa kuajiriwa, wala si mmoja wa kikundi cha manabii. Mimi ni mchungaji na mtunza mikuyu.
15. Mwenyezi-Mungu alinitoa katika kazi yangu hiyo ya uchungaji, akaniamuru nije kuwaambia unabii watu wake wa Israeli.