Amosi 7:3-8 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Basi, Bwana Mwenyezi-Mungu akabadili nia yake,akasema, “Haitakuwa hivyo!”

4. Bwana Mwenyezi-Mungu alinijalia maono mengine: Nilimwona Bwana Mwenyezi-Mungu akiuita moto wa hukumu ya kuwaadhibu watu. Moto huo uliunguza vilindi vikuu vya bahari, ukaanza kuiteketeza nchi kavu.

5. Ndipo nikasema:“Ee Bwana Mwenyezi-Mungu, nakusihi uache kuadhibu!Wazawa wa Yakobo watawezaje kuishi?Wao ni wadogo mno!”

6. Basi, Mwenyezi-Mungu akabadili nia yake,akasema: “Hili pia halitatukia.”

7. Mwenyezi-Mungu alinijalia tena maono mengine: Nilimwona Mwenyezi-Mungu amesimama karibu na ukuta, ameshika mkononi mwake uzi wenye timazi.

8. Naye akaniuliza: “Amosi, unaona nini?” Nikamjibu, “Naona timazi.” Kisha Mwenyezi-Mungu akasema:“Tazama! Naweka timazi kati ya watu wangu Waisraeli.Sitavumilia tena maovu yao.

Amosi 7