13. Usitoe tena unabii hapa mjini Betheli, kwa kuwa hapa ni maskani ya ibada ya mfalme; ni hekalu la utawala huu.”
14. Amosi akamjibu Amazia, “Mimi si nabii wa kuajiriwa, wala si mmoja wa kikundi cha manabii. Mimi ni mchungaji na mtunza mikuyu.
15. Mwenyezi-Mungu alinitoa katika kazi yangu hiyo ya uchungaji, akaniamuru nije kuwaambia unabii watu wake wa Israeli.
16. Nawe basi, ewe Amazia,sikiliza neno la Mwenyezi-Mungu:Wewe waniambia nisitoe unabii dhidi ya Israeli,wala nisihubiri dhidi ya wazawa wa Isaka.
17. Kwa hiyo, Mwenyezi-Mungu asema hivi:‘Mkeo atakuwa malaya mjini,na wanao wa kiume na kike watauawa vitani.Ardhi yako itagawanywa na kupewa wengine,nawe binafsi utafia katika nchi najisi,nao Waisraeli hakika watapelekwa uhamishoni,mbali kabisa na nchi yao.’”