11. Nyinyi mnawakandamiza fukarana kuwatoza kodi ya ngano kupita kiasi.Mnajijengea nyumba za mawe ya kuchonga,lakini nyinyi hamtaishi humo;mnalima bustani nzuri za mizabibu,lakini hamtakunywa divai yake.
12. Maana mimi najua wingi wa makosa yenuna ukubwa wa dhambi zenu;nyinyi mnawatesa watu wema,mnapokea rushwana kuzuia fukara wasipate haki mahakamani.
13. Basi, kutakuwa na wakati mbayaambao hata mwenye busara atanyamaza.
14. Tafuteni kutenda mema na si mabaya,ili nyinyi mpate kuishinaye Mwenyezi-Mungu wa majeshiawe pamoja nanyi kama mnavyosema.
15. Chukieni uovu, pendeni wema,na kudumisha haki mahakamani.Yamkini Mwenyezi-Mungu wa majeshi atawafadhili watu wa Yosefu waliobaki.
16. Basi, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa majeshi,naam, Mwenyezi-Mungu asema:“Patakuwa na kilio kila mahali mitaani;watu wataomboleza: ‘Ole! Ole!’Wakulima wataitwa waje kuomboleza,na mabingwa wa kuomboleza waje kufanya matanga.
17. Patakuwa na kilio katika mashamba yote ya mizabibu;maana nitapita kati yenu kuwaadhibu.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.”
18. Ole wenu nyinyi mnaoingojea kwa hamusiku ya Mwenyezi-Mungu!Kwa nini mnaitaka sana siku hiyo?Siku hiyo, itakuwa siku ya giza na sio ya mwanga!
19. Mambo yatakuwa kama mtu aliyekimbia simba,halafu akakumbana na dubu!Au kama mtu anayerudi nyumbani kwake,akatia mkono ukutani, akaumwa na nyoka.
20. Siku ya Mwenyezi-Mungu itakuwa giza, na sio mwanga;itakuwa huzuni bila uangavu wowote.
21. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Nazichukia na kuzidharau sikukuu zenu;siifurahii mikutano yenu ya kidini.
22. Mjaponitolea sadaka zenu za kuteketezwa na za nafaka,mimi sitakubali kuzipokea;na sadaka zenu za amani za wanyama wanonomimi sitaziangalia kabisa.
23. Ondoeni mbele yangu kelele za nyimbo zenu!Sitaki kusikiliza muziki wa vinubi vyenu!
24. Lakini acheni haki itiririke kama maji,uadilifu uwe kama mto usiokauka.
25. “Enyi Waisraeli, wakati ule mlipokuwa kule jangwani kwa miaka arubaini, je, mliniletea tambiko na sadaka hata mara moja?
26. Je, wakati huo mlibeba kama sasa vinyago vya mungu wenu Sakuthi mfalme wenu na vinyago vya Kaiwani mungu wenu wa nyota, vitu ambavyo mlijitengenezea wenyewe?
27. Kwa hiyo nitawapeleka uhamishoni, mbali kuliko Damasko! Hayo amesema Mwenyezi-Mungu, ambaye jina lake ni Mungu wa Majeshi.