9. “Niliwapiga pigo la ukame na ukungu;nikakausha bustani na mashamba yenu ya mizabibu;nzige wakala mitini na mizeituni yenu.Hata hivyo hamkunirudia.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
10. “Niliwaleteeni ugonjwa wa taunikama ule nilioupelekea Misri.Niliwaua vijana wenu vitani,nikawachukua farasi wenu wa vita.Maiti zilijaa katika kambi zenu,uvundo wake ukajaa katika pua zenu.Hata hivyo hamkunirudia.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
11. “Niliwaangusha baadhi yenu kwa maangamizikama nilivyoangamiza Sodoma na Gomora.Wale walionusurika miongoni mwenu,walikuwa kama kijiti kilichookolewa motoni.Hata hivyo hamkunirudia.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.