Amosi 2:4-7 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu wa Yuda wametenda dhambi tena na tena,kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.Wamepuuza sheria zangu,wala hawakufuata amri zangu.Wamepotoshwa na miungu ileile waliyoihudumia wazee wao.

5. Basi, nitaishushia moto nchi ya Yuda,na kuziteketeza kabisa ngome za Yerusalemu.”

6. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Waisraeli wametenda dhambi tena na tena,kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.Wamewauza watu waaminifukwa kuwa hawakuweza kulipa madeni yao;na kuwauza watu fukarawasioweza kulipa deni la kandambili.

7. Huwanyanyasa na kuwakandamiza wanyonge,na maskini huwabagua wasipate haki zao.Mtu na baba yake hulala na mjakazi yuleyule,hivyo hulitia unajisi jina langu takatifu.

Amosi 2