Amosi 1:5-10 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Nitayavunjavunja malango ya mji wa Damasko,na kuwang'oa wakazi wa bonde la Aweni,pamoja na mtawala wa Beth-edeni.Watu wa Aramu watapelekwa uhamishoni Kiri.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

6. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu wa Gaza wametenda dhambi tena na tena,kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.Walichukua mateka watu kabila zima,wakawauza wawe watumwa kwa Waedomu.

7. Basi, nitazishushia moto kuta za mji wa Gaza,nao utaziteketeza kabisa ngome zake.

8. Nitawang'oa wakazi wa mji wa Ashdodi,pamoja na mtawala wa Ashkeloni.Nitanyosha mkono dhidi ya Ekroni,nao Wafilisti wote waliosalia wataangamia.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

9. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu wa Tiro wametenda dhambi tena na tena,kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.Walichukua mateka kabila zima hadi Edomu,wakaukiuka mkataba wa urafiki waliokuwa wamefanya.

10. Basi, nitazishushia moto kuta za mji wa Tiro,na kuziteketeza kabisa ngome zake.”

Amosi 1