40. Wewe ulinijalia nguvu ya kupigana vita;uliwaporomosha adui chini yangu.
41. Uliwafanya adui zangu wakimbie,na wale walionichukia niliwaangamiza.
42. Walitafuta msaada, lakini hapakuwa na wa kuwaokoa,walimlilia Mwenyezi-Mungu, lakini hakuwajibu.
43. Niliwatwanga na kuwaponda kama mavumbi ya nchi,nikawaponda na kuwakanyaga kama matope barabarani.
44. “Wewe uliniokoa na mashambulizi ya watu wangu,umenifanya mtawala wa mataifa.Watu nisiowajua walinitumikia.
45. Wageni walinijia wakinyenyekea,mara waliposikia habari zangu walinitii.