38. Niliwafuatia adui zangu na kuwaangamiza,sikurudi nyuma mpaka wameangamizwa.
39. Niliwaangamiza, nikawaangusha chiniwasiweze kuinuka tena;walianguka chini ya miguu yangu.
40. Wewe ulinijalia nguvu ya kupigana vita;uliwaporomosha adui chini yangu.
41. Uliwafanya adui zangu wakimbie,na wale walionichukia niliwaangamiza.
42. Walitafuta msaada, lakini hapakuwa na wa kuwaokoa,walimlilia Mwenyezi-Mungu, lakini hakuwajibu.
43. Niliwatwanga na kuwaponda kama mavumbi ya nchi,nikawaponda na kuwakanyaga kama matope barabarani.
44. “Wewe uliniokoa na mashambulizi ya watu wangu,umenifanya mtawala wa mataifa.Watu nisiowajua walinitumikia.