2 Samueli 22:25-33 Biblia Habari Njema (BHN)

25. Mwenyezi-Mungu amenituza kadiri ya uadilifu wangu,yeye anajua usafi wangu.

26. “Wewe ni mwaminifu kwa walio waaminifu,mwema kwa wale walio wema.

27. Wewe ni mkamilifu kwa walio wakamilifu,lakini mkatili kwa watu walio waovu.

28. Wewe wawaokoa walio wanyenyekevu,lakini wawaangalia wenye majivuno kuwaporomosha.

29. Ee Mwenyezi-Mungu, wewe u taa yangu,Mungu wangu, unayefukuza giza langu.

30. Kwa msaada wako, wakishambulia kikosi;wewe wanipa nguvu ya kuruka kuta zake.

31. Anachofanya Mungu hakina dosari!Ahadi ya Mwenyezi-Mungu ni ya kuaminika;yeye ni ngao kwa wote wanaomkimbilia.

32. “Nani aliye Mungu isipokuwa Mwenyezi-Mungu?Nani aliye mwamba wa usalama ila Mungu wetu?

33. Mungu huyu ndiye kimbilio langu imara,na ameifanya njia yangu iwe salama.

2 Samueli 22