4. Chumba cha sehemu ya kuingilia kilikuwa na urefu wa mita 9, sawa na upana wa nyumba hiyo, na kimo chake mita 54. Kuta zake zilifunikwa kwa dhahabu safi upande wa ndani.
5. Ukumbi ulizungushiwa mbao za miberoshi na kufunikwa kwa dhahabu safi na kuchorwa mifano ya miti ya mitende na minyororo.
6. Mfalme Solomoni aliipamba nyumba ya Mwenyezi-Mungu kwa mawe mazuri ya thamani. Dhahabu aliyotumia ilitoka nchi ya Parvaimu.
7. Aliifunika nyumba yote kwa dhahabu: Boriti zake, vizingiti vyake, kuta zake na milango yake. Kutani palichongwa viumbe wenye mabawa.