2 Mambo Ya Nyakati 23:10-14 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Kisha, akawapanga watu wote kuanzia upande wa kusini mpaka upande wa kaskazini wa nyumba na kuzunguka madhabahu na nyumba, kila mmoja silaha yake mkononi, ili kumlinda mfalme.

11. Halafu wakamtoa nje mwana wa mfalme, wakamvika taji kichwani, na kumpa ule ushuhuda; wakamtawaza nao Yehoyada na wanawe wakampaka mafuta awe mfalme, kisha watu wakashangilia wakisema, “Aishi mfalme!”

12. Naye Malkia Athalia aliposikia sauti za watu wakikimbia na kumshangilia mfalme aliwaendea hao watu waliokuwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.

13. Alipochungulia akamwona mfalme mpya amesimama karibu na nguzo kwenye lango, huku makapteni na wapiga tarumbeta wakiwa kando ya mfalme na wakazi wote wakishangilia na kupiga tarumbeta; nao waimbaji wakiwa na ala zao za muziki wakiongoza watu katika sherehe; ndipo aliporarua nguo zake na kusema kwa sauti kubwa “Uhaini! Uhaini!”

14. Kisha kuhani Yehoyada aliwatoa nje makapteni wa jeshi akisema mtoeni nje katikati ya askari; yeyote atakayemfuata na auawe kwa upanga. Kwa sababu alisema “Msimuulie katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.”

2 Mambo Ya Nyakati 23