1 Wathesalonike 5:24-27 Biblia Habari Njema (BHN)

24. Yeye anayewaita nyinyi atafanya hivyo kwani ni mwaminifu.

25. Ndugu, tuombeeni na sisi pia.

26. Wasalimuni ndugu wote kwa ishara ya upendo.

27. Nawahimizeni kwa jina la Bwana muwasomee ndugu zetu wote barua hii.

1 Wathesalonike 5