1 Wathesalonike 4:7-10 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Mungu hakutuita tuishi maisha ya zinaa, bali tuishi katika utakatifu.

8. Kwa hiyo basi, anayedharau mafundisho hayo hamdharau mtu, bali anamdharau Mungu mwenyewe anayewapeni Roho wake Mtakatifu.

9. Hakuna haja ya kuwaandikieni juu ya kuwapenda ndugu zenu waumini. Nyinyi wenyewe mmefundishwa na Mungu namna mnavyopaswa kupendana.

10. Na mmekuwa mkiwatendea hivyo ndugu zenu wote kila mahali katika Makedonia. Basi, ndugu, tunawaombeni mfanye hata zaidi.

1 Wathesalonike 4