1 Wakorintho 7:37-40 Biblia Habari Njema (BHN)

37. Lakini kama huyo mwanamume akiamua kwa hiari moyoni mwake kutooa na kama anaweza kuzitawala tamaa zake na kuamua namna ya kufanya, basi, anafanya vizuri zaidi asipomwoa huyo mwenzake bikira.

38. Kwa maneno mengine: Yule anayeamua kuoa anafanya vema; naye anayeamua kutooa anafanya vema zaidi.

39. Mwanamke aliyeolewa huwa amefungwa na mumewe kwa muda wote mumewe aishipo. Lakini mumewe akifa, mama huyo yuko huru, na akipenda anaweza kuolewa na mtu yeyote, mradi tu iwe Kikristo.

40. Lakini, nionavyo mimi, atakuwa na heri zaidi kama akibaki hivyo alivyo. Hayo ni maoni yangu, na nafikiri mimi pia ninaye Roho wa Mungu.

1 Wakorintho 7