1 Wafalme 8:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Basi, mfalme Solomoni akawakutanisha mbele yake huko Yerusalemu wazee na viongozi wote wa makabila na wa koo za Israeli ili waliondoe sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu katika mji wa Daudi, yaani Siyoni.

2. Wakati wa sikukuu ya mwezi wa Ethanimu, yaani mwezi wa saba. Ndipo watu hao wote walipokusanyika mbele ya mfalme Solomoni.

3. Baada ya wazee wote wa Israeli kuwasili, makuhani walibeba sanduku la agano.

1 Wafalme 8