1 Timotheo 2:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kwanza kabisa, nawasihi muombe dua, msali na kumshukuru Mungu kwa ajili ya watu wote,

2. kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi maisha ya utulivu na amani pamoja na uchaji wa Mungu na mwenendo mwema.

3. Jambo hili ni jema na lampendeza Mungu Mwokozi wetu,

4. ambaye anataka watu wote waokolewe na wapate kuujua ukweli.

5. Maana yuko Mungu mmoja, na pia yuko mmoja anayewapatanisha watu na Mungu, binadamu Kristo Yesu,

1 Timotheo 2