1 Petro 2:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Basi, acheni uovu wote; uongo, unafiki, wivu na maneno ya kashfa visiweko tena.

2. Kama vile watoto wachanga wanavyotamani maziwa, nanyi pia mnapaswa kuwa na hamu ya maziwa halisi ya kiroho, ili kwa nguvu yake mpate kukua na kukombolewa.

3. Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Mmegundua kwamba Bwana ni mwema.”

4. Basi, mwendeeni Bwana! Yeye ndiye jiwe hai lililokataliwa na watu; lakini mbele ya Mungu ni jiwe teule na la thamani kubwa.

5. Mwendeeni yeye kama mawe hai mkajengeke na kuwa nyumba ya kiroho ambamo mtatumikia kama makuhani watakatifu, kutolea tambiko za kiroho zenye kumpendeza Mungu kwa njia ya Yesu Kristo.

1 Petro 2